Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askari JTWZ mbaroni tuhuma za kumuua mkewe kisa wivu mapenzi

Pwani Ed Askari JTWZ mbaroni tuhuma za kumuua mkewe kisa wivu mapenzi

Sat, 1 May 2021 Chanzo: ippmedia.com

Magiladi ambaye ni askari wa Kikosi cha Jeshi Namba 36 (36 KJ) anadaiwa kumuua mkewe huyo ambaye alikuwa mkazi wa Mwanalugali Kata ya Tumbi, wilayani Kibaha kwa madai ya kufanya tendo la ndoa nje ndoa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa, alisema tukio hilo lilitokea Aprili 25, mwaka huu, majira ya saa 4:00 usiku eneo la Mwanalugali. Alisema Fatuma alifariki dunia akiwa njiani kwenda Hospitali ya Tumbi kwa ajili ya matibabu.

Wankyo alisema mtuhumiwa amekamatwa baada ya tukio hilo na mahojiano yanaendelea na upelelezi ukakamilika,atafikishwa mahakamani.

Alisema baada ya kufanya tukio hilo, mtuhumiwa alikimbia na kumwacha mke wake, ambaye sasa ni marehemu, akiwa chini hadi wasamaria wema walipojitokeza na kumchukua kumpeleka hospitalini.

Katika tukio lingine, mwanamke mmoja (jina linahifadhiwa) ambaye alikuwa mfanyabiashara wa pombe za kienyeji aliokotwa akiwa amefariki dunia katika mazingira ya kutatanisha.

Kamanda Wankyo alisema kabla ya kifo, Aprili 25 usiku wa manane akiwa na mama yake mzazi wakitokea katika kilabu chao cha kuuzia pombe, walirudi nyumbani kwa mama yake.

Alisema baadaye mwanamke huyo aliaga kutoka kwa mama yake kwenda kwake na hakufika mpaka alipookotwa pembezoni mwa barabara akiwa amefariki dunia kwa kunyongwa shingo.

Jeshi la Polisi linawashikilia watu 17 wanaohusishwa na tukio hilo ambao wanaendelea kuhojiwa.

Chanzo: ippmedia.com