Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ashtakiwa kwa kudanganya ukubwa wa ‘baga’ kwenye tangazo

Baga.jpeg Ashtakiwa kwa kudanganya ukubwa wa ‘baga’ kwenye tangazo

Wed, 30 Aug 2023 Chanzo: Mwananchi

Mahakama nchini Marekani imemkuta na kesi ya kujibu mmiliki wa kampuni ya Burger King inayohusika na kutengeneza vyakula mbalimbali kwa tuhuma za kudangaya wateja ukubwa wa ‘baga’ kwenye picha tofauti na uhalisia ulivyo.

Pia kampuni hiyo inatuhumiwa kuwapotosha wateja kwa kuwaonyesha baga yenye nyama nyingi katika ‘menyu’ yake tofauti na uhalisia ulivyo ukiinunua.

Aidha, kampuni hiyo imekanusha madai hayo na kuyaiota ni ya uongo; "Madai ya walalamikaji ni ya uongo,"

"Nyama ya ng'ombe iliyopo katika picha za matangazo yetu ni sawa na zinazotumiwa," amesema msemaji wa Burger King katika taarifa yao.

Minyororo mingine ya vyakula vya haraka hivi majuzi imekabiliwa na changamoto za kisheria juu ya madai ya utangazaji wa uwongo.

Kesi kama hiyo imewahi kuzikuta kampuni mbalimbali za vyakula duniani kwa kutuhumiwa kudanganya kinachoonyeshwa katika matangazo na uhalisia, miongoni mwa kampuni hizo ni pamoja na; McDonald na Wendy.

Mwaka 2022 kampuni hizo zilishitakiwa kwa kuongeza ukubwa wa asilimia 15% katika bidhaa zao tofauti na uhalisia wake.

Chanzo: Mwananchi