Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kukutwa na nyama ya wanyamapori

76660 Nyamapic

Sun, 22 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma . Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia Jonathan Temu (41)mkazi wa Area A mkoani humo kwa kukutwa na nyama ya nsya wanne na digidigi mmoja wenye thamani ya Sh2.8 milioni.

Akizungumza leo Jumamosi Septemba 21, 2019 Kamanda wa Polisi mkoani humo, Gilles Muroto amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa jana.

Amesema Temu alihifadhi nyama hiyo katika mifuko ya plastiki na kuweka katika boksi kisha kusafirisha katika basi linalofanya safari kati ya Mkoa wa Singida na Dodoma.

Muroto amesema uchunguzi zaidi unafanyika ili kubani silaha iliyotumika katika uwindaji wa wanyamapori hao, mara upelelezi utakapokamilika atafikishwa mahakamani.

Chanzo: mwananchi.co.tz