Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ashikiliwa kwa kupatikanana risasi 39

Risasi Riffle (600 X 303) Ashikiliwa kwa kupatikanana risasi 39

Tue, 22 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la polisi mkoani Mara linamshikilia mtu mmoja kwa tuhuma za kupatikana na risasi 39 za bunduki aina ya riffle pamoja na nyamapori kinyume cha sharia.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kukamatwa kati ya Mwezi Julai na Agosti mwaka huu akiwa ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa upande wa wilaya ya Bunda akiwa anafanya uwindaji haramu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Salim Morcase amebainishwa hayo leo Jumanne Agosti 22, 2023 wakati akizungumza waandishi wa habari ambapo amesema kuwa kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kunatokana na operesheni inayondeshwa na jeshi hilo ndani ya mkoa kwa lengo la kutokomeza uhalifu na wahalifu.

"Katika operesheni hii tumebaini jumla ya wanyamapori 21 waliuwawa hivyo basi mbali na huyu mtuhumiwa aliyekamatwa akiwa na risasi na nyamapori pia tumefanikiwa kuwakamta watuhumiwa wengine 37 kwa kukutwa na nyara za serikali na tayari wote wamefikishwa mahakamani," amesema Morcase

Amesema jeshi hilo pia limebaini uwepo wa mtandao wa watu wanaojihusisha na wizi wa pikipiki kutika katika mikoa mbalimbali nchini na kuzileta katika mikoa iliyopo mipakani, Mara ikiwa ni mmojawapo.

"Mtandao huu unawashirikisha watanzania pamoja na wenzao wa nchi jirani na soko kuu la pikipiki hizo za wizi lipo nchi jirani hapa tayari tumemkamata na raia wa kigeni pia," amesema

Amefafanua kuwa jumla ya watuhumiwa 16 wanashikiliwa na jeshi hilo kwa tuhuma za kujihisisha na mtandao huo huku pikipiki 27 zikiwa zimekamatwa na kwamba oparesheni hiyo bado inaendelea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live