Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ashikiliwa kwa kuchoma gari mkoani Mbeya

3130f33dde231579eac46e4b65587d6e Ashikiliwa kwa kuchoma gari mkoani Mbeya

Sat, 12 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linamshikilia Sam Likwelile (29) mkazi wa Gombe jijini humo kwa tuhuma za kuchoma moto gari lenye namba za usajili T 281 CZP Toyota IST mali ya Salome Samson.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei imesema kuwa mnamo Desemba 18, 2020 majira ya 2;30 usiku katika Mtaa wa Majengo Mapya, Kata ya Nsalaga, Tarafa ya Iyunga jijini humo, mtuhumiwa huyo alivunja kioo cha gari hilo na kisha kuchoma moto sehemu ya ndani ya gari hilo na kisha kukimbia.

“Katika mahojiano yaliyofanyika mtuhumiwa amekiri kutenda kosa hilo na upelelezi bado unaendelea na ukishakamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria” amesema Matei.

Katika hatua nyingine Matei amesema kuwa jeshi hilo linamshikilia Rhoda Somora (66) mkazi wa Itezi mkoani humo baada ya kukamatawa na pombe haranu ya gongo lita 25 kutokana na misako mbalimbali inayoendela kufanywa.

Chanzo: habarileo.co.tz