Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ashambuliwa akiwa nyumbani kwa mtalaka wake

Mtalaka Shmabulio.png Ashambuliwa akiwa nyumbani kwa mtalaka wake

Fri, 29 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Selemani Kizito, Mkazi wa Mtaa wa Mmingano, Kata ya Tandika, Manispaa ya Mtwara Mikindani, ameshambuliwa kwa kupigwa mawe na kuchanwa na wembe akiwa nyumbani kwa mtalaka wake.

Inadaiwa Kizito alifika nyumbani hapo kwa lengo la kumpeleka mtoto kwa mama yake, na ndipo aliposhambuliwa na mtu anayedhaniwa kuwa na uhusiano na mtalaka wake.

Akizungumza nyumbani kwake leo, Desemba 29, 2023 amesema mwanamke huyo alikuwa mkewe wa ndoa, lakini walitengana zaidi ya miaka miwili iliyopita wakiwa na mtoto mmoja wa kike.

Kwa mujibu wa Kizito, mtalaka wake huyo alihitaji kumuona mtoto ndipo akampigia simu akiomba ampeleke mtoto huyo ili amuone.

“Mama yake alinipigia simu kuwa nimpeleke mtoto akamuone, nilipofika na baada ya kumuona akasema niondoke naye, mimi nikamuambia nimuache kisha nitamfuata siku nyingine kumchukua,” amesema Kizito na kuongeza;

“Baadaye mama wa mtoto akawa anaongea na simu, ndipo akaja mtu ambaye simfahamu akaanza kunishambulia kwa kunichana na usoni na wembe, kisha akanipiga na jiwe eneo la jicho,” amesema.

Zainabu Dadi, mama mzazi wa Kizito, amesema kijana wake amepigwa na kuumizwa katika maeneo mbalimbali mwilini bila kuwa na kosa lolote.

“Nikiwa nyumbani niliitwa na majirani kuwa mwanangu amepigwa, nilikimbia kwenda eneo la tukio nilikuta akiwa na hali mbaya akiwa hajitambui ndio tukamuwahisha hospitalini,” amesema.

Nae Subira Seleman (dada wa majeruhi) amesema: “Kaka yake aliaga kuwa anampeleka mtoto kwa mama yake na hapakuwa na ugomvi kati yao…kilichomkuta kaka yangu kiukweli kimeniumiza na sijakipenda.”

“Toka ametengana na mkewe, tumekuwa tukiishi na mtoto, jana tu ndiyo mama yake akiomba apelekewe, ndiyo kaka akamchukua mtoto na kumpeleka ili mama mtu amuone mtoto wake.”

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mtwara, Nikocodemus Katembo amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba wanawatafuta watu waliohusika na tukio hilo wachukuliwe hatua.

Amesema Desemba 26, 2023 watu wanaofahamika kwa sura, walimshambulia mwananchi ajulikanaye kwa jina la Rajabu kwa kutumia vipande vya mawe na kumsababishia majeraha mbalimbali mwilini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live