Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Asakwa kwa tuhuma wizi wa injini za pikipiki kampuni ya Mohammed Enterprises

66982 Pikipikipic

Tue, 16 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.  Kampuni ya Mohammed Enterprises inamsaka mmoja wa wafanyakazi wake kwa tuhuma za kuiba injini 172 za pikipiki za kampuni hiyo.

Hayo yameelezwa leo Jumanne Julai 16, 2019 katika tangazo kwa umma lililotolewa na kampuni hiyo.

Tangazo hilo limemtaja mtuhumiwa huyo na kubainisha kuwa amefanya wizi huo Juni 15, 2019.

“Tukio hili limeripotiwa katika kituo cha polisi cha Chang’ombe na kupewa kumbukumbu namba CAG/IR/7557/2019,” linaeleza huku likitaja namba za injini hizo.

 

 

Pia Soma



Chanzo: mwananchi.co.tz