Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aquilina abakwa na kuuawa

RPC MUTAFUNGWA WEB 660x400 Aquilina abakwa na kuuawa

Tue, 4 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aquilina Godfrey Martin mwenye umri wa miaka 17 alikutwa akiwa amefariki na mwili wake kutupwa kwenye uchochoro katika mtaa wa Nyamanoro mashariki wilaya ya Ilemela jijini Mwanza

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Wilbrod Mutafungwa amesema tukio hilo limetokea tarehe 27 ya mwezi uliopita ambapo mwili huo uliokutwa kwenye uchochoro huo majira ya saa kumi na mbili alfajiri ukiwa umefunikwa huku sehemu ya mwili wake ukiwa wazi

Aidha kamanda Mutafungwa amesema hadi sasa watu wawili Jovin Kamando miaka 26 na Kalvin Raymond miaka 27 ambao ni wapenzi wa binti huyo wanashikiliwa kwa tuhuma za mauaji ya binti huyo ambayo chanzo chake kinadaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi

Mara baada ya mwili huyo kufanyiwa uchunguzi ulikabidhiwa kwa ndugu zake kwa ajili ya mazishi wakati uchunguzi wa mauaji hayo yakiendelea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live