Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Apigwa miaka 15 jela kwa kumbaka raia wa kigeni

3af90c33da689c3157562c19a29f2000.png Apigwa miaka 15 jela kwa kumbaka raia wa kigeni

Wed, 8 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa limesema Mahakama ya Hakimu Mkazi ya mkoa huo imemhukumu kijana Selemani Juma (36) kifungo cha miaka 45 jela, baada ya kupatikana na hatia ya unyang’anyi na kubaka.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi alisema Juma alidaiwa kumbaka msichana raia wa Ujerumani (jina limehifadhiwa) Desemba 2, mwaka jana.

Kamanda Bukumbi aliwaeleza waandishi wa habari jana kuwa baada ya Juma kutenda kitendo hicho alimpora msichana huyo simu na fedha Sh 100,000 na akakimbia.

"Baada ya tukio kutokea na kuripotiwa kituo cha polisi hatua za haraka za uchunguzi zilifanyika na kupelekea mtuhumiwa huyo kukamatwa na hatimaye kufikishwa mahakamani," alisema.

Kamanda Bukumbi alisema Oktoba 19 mwaka huu Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Iringa ilimtia hatiani kijana huyo kumhukumu kifungo cha miaka 45 jela na fidia ya Sh milioni moja.

Wakati huo huo alisema kwa nyakati tofauti polisi walikamata watu watatu wakiwa na meno matatu ya tembo na vipande viwili.

Kamanda Bukumbi alisema Novemba 26, mwaka huu saa 7:45 usiku katika Kijiji cha Mapogoro wilayani Iringa, jeshi hilo liliwakamata watu wawili (majina yao yamehifadhiwa) wakiwa na meno mawili ya tembo na vipande viwili vidogo.

Alisema katika tukio lingine Desemba 5, 2021 katika maeneo ya Posta mjini Iringa, polisi kwa kushirikiana na askari wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, walimkamata mtu (jina limehifadhiwa) akiwa na jino moja la tembo.

Kamanda Bukumbi alisema watuhumiwa watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi wa matukio kukamilika.

Alisema pia watoto 22 wamekamatwa wakituhumiwa kushiriki katika matukio ya uhalifu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live