Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Apigwa faini ya Tsh. 500,000 kwa kuishi nchini bila kibali

Faini Pc Data Alimwa faini ya Sh500,000 kwa kuishi nchini bila kibali

Tue, 12 Oct 2021 Chanzo: mwananchidigital

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu raia wa Liberia, Aloysious Blam kulipa faini ya Sh500,000 au kwenda jela miezi sita, baada ya kupatikana na hatia ya kuishi nchini bila kibali.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba, baada ya mshtakiwa kukiri shitaka lake.

Akisoma hukumu hiyo leo Oktoba 11, Hakimu Simba amesema mshtakiwa anamtia hatiani kama alivyoshtakiwa.

"Mahakama imekutia hatiani hivyo, inakuhukumu kulipa faini ya Sh500,000 na ukishindwa ni kwenda jela mwaka mmoja," amesema hakimu Simba.

Kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo, Wakili kutoka Idara uhamiaji, Sitta Shija ameiomba mahakama itoe adhabu kali kwa mshtakiwa ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hivyo.

Kabla ya kutolewa hukumu hiyo, mshtakiwa ameomba mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa anategemewa na familia yake.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo ameshindwa kulipa faini hiyo na hivyo kutumikia kifungo hicho.

Katika kesi ya msingi, mshtakiwa anadaiwa kutenda kosa hilo Septemba 7, 2021 baada ya kukamatwa na kuhifadhiwa katika kituo cha Polisi Oysterbay, akidaiwa raia wa Liberia aliyekuwa akiishi nchini bila kuwa na kibali, jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Mshtakiwa baada ya kukamatwa alihojiwa na maofisa was Idara ya Uhamiaji na kisha kufikishwa mahakamani

Chanzo: mwananchidigital