Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Apigwa faini kwa kujiunganishia maji kinyemela

MAJI KINYEMELA Apigwa faini kwa kujiunganishia maji kinyemela

Tue, 18 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama (KUWASA) imemtoza fidia ya shilingi milioni 1.2 mteja aliyeamua kujiunganishia huduma ya maji kwa kuchepusha (bypass) katika makazi yake.

Mteja huyo kwa jina Hamis Omari amekutwa kajiunganishia maji ambayo hayapiti katika Dira na kuyaelekeza katika maliwato na kuyatumia kwa kazi mbalimbali za nyumbani.

Ni kosa kuharibu miundombinu ya maji/kujiunganishia kwa mujibu wa Sheria Na. 5 ya mwaka 2019, Sheria ya Huduma ya maji na Usafi wa Mazingira

Bwana Hamisi Omari ni mkazi wa Mtaa wa Mwime Kata ya Mwendakulima

Katika wiki nne za mwezi Juni, 2023 Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama ( KUWASA ) imekamata wananchi wawili kwa uharibifu wa miundombinu ya usambazaji majisafi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live