Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Apigwa akidaiwa kutaka kumuua mkewe kwa mamba

Mamba Apigwa akidaiwa kutaka kumuua mkewe kwa mamba

Wed, 31 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkazi wa Kijiji cha Kiyogo kilichopo Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe, Lucas Mahundi amenusurika kifo baada kupigwa na kujeruhiwa na Watoto wake wawili wakimtuhumu kumtuma mamba kishirikina ili amuue Mama yao November 2022.

Akisimulia kilichomtokea Lucas amesema “Batazari alinipiga na fimbo kwenye paji la uso nikadondoka nikasema wataniua hawa Mabwana, nikasimama na kukimbia huku napiga kelele nilipofika hatua 10 kwasababu alishika gongo refu akanipiga tena nikaanguka mwingine akaja kunipiga na panga mgongoni"

Licha ya Mahundi kukataa tuhuma hizo mbele ya mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Ludewa, Deogratius Massawe, baadhi ya Wananchi akiwemo Adriano Luena amemtaka Mahundi kuwa muwazi kuhusu kifo cha Mkewe kwakuwa Watoto wake walijaribu kumuua mara kadhaa kwakuwa kifo cha Mama yao kilikuwa na mashaka “Inawezekana vipi mamba amuue Mtu bila kumla, huyo mamba hakuwa na njaa?”

Masawe amefika katika Kijiji hicho ili kutoa elimu na kuwataka Wananchi wasijchukulie sheria mkononi “Serikali haiamini uchawi ila kuna sheria ya uchawi maana yake mambo hayo yapo, Mtu akifanya hivyo vitendo tukiwa na ushahidi akamatwe apelekwe Mahakamani na atafungwa kuna sheria inaitwa The witch craft act sura ya 18 katika sheria za Tanzania"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live