Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Apandishwa kizimbani kwa kumtorosha mtuhumiwa

15848 Pic+kizimbani TanzaniaWeb

Thu, 6 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkazi wa Kinondoni, Godfrey Benjamini amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Mwanzo Kinondoni akidaiwa kumtorosha mtuhumiwa Francis Benjamini ambaye ni mdogo wake.

Mwendesha mashtaka wa Serikali, January Kasekwa amedai mbele ya Hakimu, Ester Kihiyo kuwa tarehe isiyofahamika Aprili mwaka huu nyakati za mchana huko Oysterbay Polisi, Godfrey alimdhamini mdogo wake Francis ili awe anaripoti katika kituo hicho cha polisi pindi anapohitajika.

Kasekwa amedai Godfrey hakufanya hivyo na badala yake alimtorosha Francis na hakumpeleka kituoni hapo kulingana na makubaliano ya sheria.

Baada ya kusomewa maelezo hayo mshtakiwa alikana na alirudishwa rumande hadi Septembaa 8 mwaka huu kesi itakapotajwa tena.

Wakati huo huo, Mkazi wa Mwenge, Jackson Ally (23) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni kwa staka la kukutwa na dawa za kulevya aina ya Heroin zenye uzito wa gramu 0.13.

Mwendesha Mashtaka, Ramadhani Mkimbu amedai mbele ya Hakimu, Frank Moshi kuwa Agosti 10 mwaka huu eneo la Mwenge mtuhumiwa huyo alikutwa na dawa hizo za kulevya.

Mshitakiwa amekana mashtaka na alirudishwa rumande hadi Septemba 18 mwaka huu kesi itakapotajwa tena.

Chanzo: mwananchi.co.tz