Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Apandishwa kizimbani kwa kumdhalilisha mtoto

Apandishwapic Udhalilishaji unazidi kushika kasi katika jamii

Mon, 28 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shaban Awadhi (52) amefikishwa mahakamani akituhumiwa kwa shambulio la aibu alilomtendea mtoto wa miaka tisa.

Mkazi huyo Igunga mjini, amefikishwa mahakama ya Hakimu Mfawidhi Wilaya ya Igunga kwa kumdhalilisha mwanafunzi wa darasa la pili.

Mwendesha Mashitaka wa Polisi Wilaya ya Igunga, Ellymajid Kweyamba ameiambia mahakama kuwa Machi 14 majira ya saa tano asubuhi katika Mtaa wa Kamando Kata ya Igunga Mjini, mshitakiwa alimshambulia mwanafunzi huyo kwa kumshika na kumvutia kwenye shamba la mahindi kisha kumvua nguo na kumwingizia kidole sehemu za siri kinyume na kifungu 138C(1)(a)(2)(b) kanuni ya adhabu sura 16 mapitio ya mwaka 2019.

Baada ya mshitakiwa kusomewa shitaka lake mbele ya Hakimu wa Wilaya ya Igunga, Lydia Ilunda alikana kosa lakini mwendesha mashitaka akaiambia mahakama kuwa upelelezi umekamilika.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 11 mshitakiwa atakapofikishwa mahakamani kusikiliza kesi yake hivyo kuendelea kubaki mahabusu.

Wakati huohuo, mkazi wa Mtaa wa Hanihani mjini Igunga, Christian Magesa (29) amepandishwa kizimbani akikabiliwa na tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi.

ADVERTISEMENT

Akimsomea shitaka hilo, Kweyamba aliiambia mahakama kuwa Machi 20, saa saba na nusu usiku katika Mtaa wa Hanihani mjini hapa, mshitakiwa Christian Magesa alikamatwa na Mkaguzi wa Polisi Melchior Fundi akiwa na gramu 35 za bangi.

Mshitakiwa alikana kutenda kosa hilo ambalo upelelezi wake umekamilika. Kesi imeahirishwa hadi Aprili 19 itakaposikilizwa na mshitakiwa yupo nje kwa dhamana ya Sh500,000 ya maneno.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live