Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Apandishwa kizimbani kwa kujaribu kumhonga Sh90 milioni Waziri Lukuvi

9785 LUKUVI+PIC TanzaniaWeb

Thu, 2 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imempandisha kizimbani Mkurugenzi wa Kampuni ya Kiluwa Steal Group and Company Ltd, Mohamed Kiluwa (50) kwa tuhuma za kutoa rushwa ya Sh90 milioni kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi.

Mshtakiwa huyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa kampuni ya Kiluwa Free Processing Zone alipandishwa kizimbani leo Agosti 2 mbele ya Hakimu mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu Huruma Shaidi na kusomewa shtaka moja la kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Akisomewa shtaka hilo mbele ya Hakimu Shaidi, Wakili wa Serikali Mkuu kutoka Takukuru, Maghela Ndimbo amedai kuwa Julai 16 mwaka huu kati ya saa sita mchana na saa nane,  mshtakiwa huyo akiwa Mkurugenzi wa kampuni hizo alitoa rushwa ya dola 40,000 sawa na Sh90 milioni fedha za kitanzania kwa Waziri Lukuvi.

Wakili Ndimbo alidai mshtakiwa huyo alitoa fedha hizo ili asiwasilishe hati za umiliki wa kiwanja namba 57 Block B Kikongo na D Disunyura vilivyopo eneo la viwanda Kibaha mkoani Pwani.

 Mshitakiwa yupo nje kwa dhamana hadi kesi itakapotajwa tena Agosti 15.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz