Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Apandishwa kizimbani kwa kuchapisha mtandaoni habari za uongo kuhusu Dk Mwakyembe

Kortinipic Data Apandishwa kizimbani kwa kuchapisha mtandaoni habari za uongo kuhusu Dk Mwakyembe

Wed, 28 Sep 2022 Chanzo: Mwananchi

Mkazi wa Ukonga, Tarzan Mwambengo amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka matano likiwemo ya kuchapisha taarifa kupitia mtandao wa YouTube, Kalomba Tv ikisema “mazishi ya Dk Mwakyembe, breaking news huzuni yatanda mazishi ya Mwakyembe aliyekuwa waziri awamu ya tano”.

Wakili wa Serikali, Amina Kombakono akisoma hati ya mashtaka amesema Agosti 9, 2022 eneo lisilojulikana ndani ya Jamuhuri wa Tanzania kupitia mtandao wa Youtube Kalambo TV, alichapisha taarifa ya “Tanzania news tumepokea habari mbaya sana kuhusu Dk Mwakyembe aliyewahi kuwa waziri” wakati akijua kuwa taarifa hiyo ni ya uongo kwa lengo la kupotosha jamii.

Katika shtaka la pili Agosti 12, 2022 akiwa eneo lisilojulikana ndani ya Jamuhuri ya Muungano kupitia akaunti yake, alichapa taarifa ambayo ilisema “mazishi ya Mwakyembe, Breaking News huzuni yatanda mazishi ya Dk Mwakyembe aliyekuwa Waziri awamu ya tano” wakati akijua taarifa hizo ni za uongo kwa lengo la kupotosha jamii.

Kombakono amedai kwamba Agosti 7, 2022 hadi Agosti 12, 2022 akiwa sehemu isiyojulikana kupitia akaunti yake, alichapisha pamoja na picha ya Dk Mwakyembe yenye ujumbe wa “Tanzania news tumepokea habari mbaya sana kuhusu Dk Mwakyembe aliyewahi kuwa waziri.”

Amesema shitaka la nne kati ya Agosti 7,2022 hadi Agosti 12,2022 eneo hilo hilo kupitia akaunti yake alisambaza taarifa ya picha ya Dk Mwakyembe iliyokuwa na ujumbe '”mazishi ya Mwakyembe aliyekuwa waziri” kwa lengo la kuleta msisimko wa hisia.

Katika shitaka la tano, amesema kati ya Januari 29, 2022 hadi Agosti 16, 2022 maeneo yasiyojulikana ndani ya Jamuhuri ya Muungano Tanzania kupitia akaunti hiyo kwa maudhui ya mtandaoni na wakati huo hana leseni kutoka mamlaka husika. Kombakono alidai upelelezi wa shauri hilo umekamilika.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate alisema dhamana ipo wazi mdhamini anatakiwa mmoja awe na kitambulisho kinachotambulikajulikana pamoja na bondi ya Sh200,000. Mshtakiwa huyo alikidhi vigezo hivyo, sasa yupo nje kwa dhamana.

Chanzo: Mwananchi