Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Apandishwa kizimbani akidaiwa kusafirisha dawa za kulevya

Mon, 29 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkazi wa Magomeni, Dar es Salaam nchini Tanzania, Ali Amiri Mlawa (34) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroine hydrochloride.

Mlawa alikamatwa Juni 1, 2019 kituo cha mabasi ubungo mawasiliano jijini Dar es Salaam.

Wakili wa Serikali ya Tanzania, Faraji Nguka akisoma shtaka linalomkabili, Mlawa mbele ya Hakimu Augustine Rwizile leo Jumatatu Julai 29, 2019 amedai mshtakiwa alikutwa na gramu 231.06 za dawa hizo ambazo ni kinyume cha sheria.

Wakili Nguka amedai upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na kuomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Rwizile alipompa nafasi mshtakiwa kuzungumza lolote amesema amekana shtaka hilo na kudai kuwa sio kweli hivyo akaomba mahakama impatie dhamana.

Hakimu Rwizile ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 13, 2019 itakapotajwa tena na mshtakiwa amepelekwa rumande kutokana na shtaka linalomkabili kutokuwa na dhamana kwa mujibu wa sheria.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz