Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Anusurika kifo kwa kucharangwa mapanga

WhatsApp Image 2022 10 10 At 4.32.24 PM.jpeg Anusurika kifo kwa kucharangwa mapanga

Tue, 11 Oct 2022 Chanzo: ippmedia

Baraka Mayala (24) mkazi wa Burugalila Kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga, amesurika kifo kwa kucharangwa mapanga kichwani na sehemu mbalimbali za mwili wake na watu ambao hawakufahamika wakati akitoka kwenye harusi. 

Tukio hilo limetokea Oktoba 7, mwaka huu majira ya saa 4 usiku.

Mayala akisimulia tukio hilo leo amesema watu hao ambao hawafahamu waliokuwa zaidi ya 10 walimvamia njiani wakati akitoka kwenye harusi majira hayo ya saa 4 usiku, na kuanza kumshambulia kwa kumkata mapanga kichwani na sehemu zingine na mwili wake na kisha kumpora kiasi cha fedha Sh. 10,000 na simu ya mkononi.

"Watu hawa walinivamia njiani nikitoka kwenye harusi kuanza kunikagua kwenye mifuko ya suruali na wakati nikijitetea ndipo wakaanga kunishambulia kwa mapanga na wamenikata kichwani mara mbili, na sehemu mbalimbali za mwili wangu kisha wakachukua Sh. 10,000 na simu ya mkononi wakakimbia"amesema Baraka.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoani Shinyanga, Dk. Kambi Buteta, amekiri kumpokea kijana huyo hosptalini hapo na kubainisha kuwa wanaendelea kumpatia matibabu.

"Tulimpokea kijana Baraka Mayala akiwa na majeraha kichwani, na sehemu mbalimbali za mwili wake, majeraha ambayo yanaashiria alijeruhiwa na kitu chenye ncha kali, lakini tulifanikiwa kumpatia huduma ya kwanza ili kuzuia damu zisiendelee kuvuja na bado anaendelea na matibabu,”amesema Dk, Buteta.

Kwa upande wake Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Jackson Mwakagonda amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kubainisha kuwa Jeshi linaendelea na upelelezi.

Chanzo: ippmedia