Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Anusurika kifo baada ya kukimbilia gari la polisi

Polisi Gari Kijana aliyenusurika kifo kwa kipigo

Wed, 20 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kijana anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 25 hadi 30 mkazi wa Kijiji cha Igoma, Kata ya Iwungilo mkoani Njombe, amenusurika kifo kutoka kwa wananchi na kukimbilia kwenye gari la polisi baada ya kukutwa na mali za wizi akizisafirisha kwa baiskeli kwenda kuziuza mjini Njombe.

Akiwa mjini Njombe katika mtaa wa Mpechi eneo la Lutilage, kijana huyo amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kuzungukwa na kundi la watu akiwemo aliyekuwa baba mwenye nyumba wake na kisha kuanza kumpa kichapo kwa madai ya kwamba amekosa maelezo ya kutosha kuhusu umiliki halali wa mali hizo.

Miongoni mwa vitu ambavyo amekutwa navyo ni pamoja na magodoro,mtungi wa gesi, TV na baiskeli ambapo miongoni mwa kundi hilo wamejitokeza watu ambao wamekirri kuwa ni vyao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live