Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Anayetuhumiwa kumuua mkewe apandishwa kizimbani

21812 Mahakamani+pic TanzaniaWeb

Fri, 12 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Anayetuhumiwa kumuua mke wake kwa sababu ya wivu wa mapenzi amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Serengeti mkoani Mara.

Mbele ya Hakimu, Ismael Ngaile, Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Renatus Zakeo alimtaja mshitakiwa kuwa ni Elisha Gimakwe (48) mkazi wa kijiji cha Borenga.

Akisoma hati ya mashitaka katika kesi ya mauaji namba 20/2018, Zakeo alidai Oktoba 7 majira ya Saa 1.30 jioni katika kijiji cha Borenga mshtakiwa alimuua Neema Gimakwe (31) ambaye ni mke wake.

Alisema mshtakiwa anakabiliwa na kosa moja la mauaji kinyume na kifungu namba 196 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Mshitakiwa hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji. Kesi imeahirishwa hadi Oktoba 24.

Chanzo: mwananchi.co.tz