Arusha. Mamia ya watu wamejitokea leo Alhamisi Machi 26, 2020 katika Mahakama ya Wilaya ya Arumeru kusikiliza kesi inayomkabili Mkami Shirima (30) anayetuhumiwa kumuua mfanyakazi wake wa ndani, Salome Zakaria(18) Machi 16, 2020.
Mtuhumiwa huyo alifikishwa mahakama akiwa kwenye ulinzi mkali huku akiwa amefunikwa sehemu kubwa ya mwili wake.
SOMA ZAIDI: Kifo cha mfanyakazi wa ndani Arusha chawaibua watetezi Mwanza
Akisoma mashtaka yanayomkabili, wakili wa Serikali Penina Joachimu amesema alifanya mauaji hayo eneo la Mianzini jijini Arusha na kwamba upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na kuomba mahakama kupanga siku nyingine ya kutajwa shauri hilo.
Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo, Amalia Mushi amesema kesi hiyo itatajwa tena Aprili 8, 2020 na mshtakiwa kurudishwa mahabusu.
Mshtakiwa huyo pia amesomewa kesi ya nyingine ya usafirishaji wa dawa za kulevya aina ya mirungi pamoja na Elias Lairien .
Pia Soma
- Wagonjwa wa corona Kenya wafikia 31
- VIDEO: Ajali ilivyoua baba na mama, watoto wao watatu wakanusurika
- Papa apimwa corona
Kesi hiyo ya kukutwa na mirungi ilitajwa kwa mara ya kwanza Septemba 24, 2019.
SOMA ZAIDI: Anayedaiwa kumuua mfanyakazi wa ndani afikishwa kortini, waandishi wazuiwa