Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Anayetapeli kwa kujifanya mshauri wa Rais akamatwa

Pingu 4 Anayetapeli kwa kujifanya mshauri wa Rais akamatwa

Wed, 21 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga linamshikilia mwanamke mmoja aliyefahamika kwa majina ya Zainabu Kagoso mkazi wa Dar es salaam (50)  aliyekuwa akijitambulisha kuwa ni mshauri wa Rais Samia Suluhu Hassan katika mambo ya kijeshi na kutumia njia hiyo kutapeli

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Henry Mwaibambe amesema kuwa mtu huyo mara baada ya kukamatwa alidai kuwa ni afisa usalama yupo Tanga kwa kazi maalum ambapo amekuja kufuatilia kazi  mbalimbali alizotumwa

"Katika oparesheni zetu tumefanikiwa kumkamata mtu mmoja mwanamke ambaye ni mkazi wa Ukonga  Dar es salaam amekuja mkoani Tanga hasa wilaya ya Kilindi akiwa anaenda ofisi mbalimbali za serikali akidai kwamba yeye ni  afisa usalama wa Taifa na amekuja  kwa kazi maalum  na kwamba yeye ni mshauri wa Rais Samia Suluhu Hassan  katika mambo ya kijeshi amekuja kuangalia kazi mbalimbali aliyotumwa tulimfuatilia na tulifanikiwa kumkamata na tumemfikisha mahakamani kwa kujifanya kuwa ni afisa wa serikali" alisema Kamanda Mwaibambe.

Aidha  katika wilaya ya Lushoto watu wanne wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kujihusisha na mauaji ya ndugu yao aliyefahamika kwa jina la  Ally Zayumba mwenye  umri wa miaka 52 aliyeuwawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani  hadi kupasuka ambapo awali taarifa ziliripotiwa na ndugu zake  katika kituo cha Polisi wilayani  humo kuwa mtu huyo amepotea na baadaye mwili wake kupatikana ukiwa umetupwa.

"Vile vile jeshi la polisi tumefanikiwa kuwakamata watu wanne na kuwafikisha mahakamani kwa tuhuma ya mauaji yaliyotokea November 14,  2022 katika kijiji cha Sunga  wilaya ya Lushoto ambapo Ally Zayumba mwenye miaka 52 aliuwawa kwa kupigwa kitu kizito kichwani na  kichwa kupasuka awali ndugu zake waliripoti kwenye kituo cha Polisi wakidai kuwa ndugu yao amepotea na hajulikani yuko wapi"

"Upelelezi wa Polisi uliendelea tulimkamata mtu mmoja anaitwa Omary Issa (25) ambaye ni ndugu wa Marehemu katika mahojiano alikiri kwamba yeye na ndugu zake wengine ndio wameshiriki  katika mauaji ya huyo ndugu yao na walikuwa tayari kwenda kutuonesha mahali walipotupa huo mwili,  na kueleza kuwa sababu za mauaji hayo wana migogoro ya kifamilia" alieleza  

Chanzo: www.tanzaniaweb.live