Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Anayelewesha Abiria kwenye Mabasi Akamatwa

14a7255974f8193f9d161a4ff8236a5c.png Polisi yamnasa mzee anayelewesha abiria kwenye Mabasi

Tue, 7 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

JESHI la Polisi Mkoa wa Mara linamshikilia Michael Abdul Said (68) mzaliwa wa Katoro mkoani Kagera kwa tuhuma za kuwalewesha abiria kwenye basi linalofanya safari kati ya Mwanza na Mara.

Matukio hayo yalishamiri mkoani humo tangu Oktoba mwaka huu ambapo watu tofauti waliripotiwa kuleweshwa na kuibiwa mali mbalimbali, huku ikihofiwa kuwa mihadarati iliyotumika ilitolewa kwa kiwango kikubwa.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, SP Longinus Tibishubwamu amesema mtuhumiwa huyo baada ya kukamatwa Disemba 02 mwaka huu, amebainisha kuwa wamekuwa wakitumia dawa ya kienyeji aina ya Kabharagata ambayo wamekuwa wakiiagiza kutoka nchini Kongo.

Amesema mtuhumiwa alikamatwa wilayani Bunda na kukiri kufanya matukio hayo katika mikoa tofauti ingawa alisema makazi yake yapo Nairobi nchini Kenya.

RPC Tibishubwamu amesema watamfikisa mahakamani wakati wowote, kwani mmoja wa abiria aliyewahi kuibiwa kwa mtindo huo katiba basi la Champion, amemtambua na mtuhumiwa amekiri kumfanyia uhalifu huo, mwezi uliopita

Chanzo: www.tanzaniaweb.live