Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Anayedaiwa msimamizi wa mali za mke wa Balali ashtakiwa kwa utakatishaji fedha

79414 Balali+pic

Thu, 10 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Elizabeth Balali (54), mfanyabiashara mkazi  wa Boko Magengeni amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka ya kujipatia Sh25 milioni kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa fedha.

Mshtakiwa huyo anayedaiwa kuwa msimamizi wa mali za mke wa  gavana wa zamani wa Benki Kuu Tanzania (BoT), marehemu Daudi Balali, amesomewa mashtaka hayo leo Alhamisi Oktoba 10, 2019 na wakili Wankyo Simon mbele ya hakimu mfawidhi, Kelvin Mhina.

Wankyo amedai kati ya Oktoba 19 na Desemba 21, 2017 jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alijipatia Sh25 milioni kwa ulaghai kutoka kwa Dk Roderick Kisenge.

Anadaiwa kumuuzia  eneo la mita 900 ambalo halijapimwa lililopo Boko Dovya wilayani Kinondoni wakati akijua si lake.

Katika shtaka la utakatishaji fedha, Wankyo amedai katika kipindi hicho  mshtakiwa alipokea Sh25 milioni kutoka kwa Dk Kisenge kupitia akaunti yake iliyopo  Benki ya CRDB wakati akijua fedha hizo ni zao la kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Elizabeth hakuruhusiwa kuongea chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza makosa ya uhujumu uchumi.

Pia Soma

Advertisement
Hakimu Mhina katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 109/2019 alimueleza mshtakiwa huyo kuwa licha ya mahakama kutokuwa na uwezo wa kuisikiliza, pia shtaka la utakatishaji wa fedha halina dhamana.

Naye  Wankyo alieleza kuwa upelelezi bado haujakamilika na kesi hiyo kuahirishwa hadi Oktoba 24, 2019 itakapotajwa tena, mshtakiwa kupelekwa rumande.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz