Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Anayedaiwa kumuua mkewe na kisha kumchoma moto, jalada lake limetuakwa DPP

98461 Pic+naomi Anayedaiwa kumuua mkewe na kisha kumchoma moto, jalada lake limetuakwa DPP

Mon, 9 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Upande wa mashtaka katika kesi ya mauaji inayomkabili Hamisi Said, ameieleza mahakama ya Kisutu, kuwa Jalada la kesi hiyo lipo kwa DPP kwa ajili ya kupitiwa na kutolewa maamuzi.

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeelezwa kuwa jalada la kesi ya mauaji inayomkabili mfanyabiashara, Hamisi Saidi(38), lipo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka Tanzania, kwa ajili ya kupitiwa na kutolewa maamuzi.

Ni baada ya upelelezi wa kesi hiyo kukamilika na hatua za uchapishaji wa jalada hilo kukamilika.

Hata hivyo, baada ya kupitiwa na kutolewa maamuzi na DPP, hatua itakayofuata ni mshtakiwa kusomewa  maelezo ya mashahidi na vielelezo(Committal Proceedings).

Said, anadaiwa kumuua Naomi Marijani, ambaye ni mke wake na kisha kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa na baadae kuchukua majivu yake na kwenda kuyafukia shambani.

Wakili wa Serikali, Janeth Magoho, ameieleza Mahakama hiyo, leo Machi 9, 2020, wakati shauri hilo lilipoitwa kwa ajili ya kutajwa.

Pia Soma

Advertisement

Magoho amedai mbele ya hakimu Mkazi Mwandamizi, Rashid Chaungu, kuwa jalada la kesi hiyo lipo kwa DPP kwa ajili ya kupitiwa na kutolewa maamuzi, hivyo anaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

“Upelelezi wa kesi hii umeshakamilika na kwa sasa lipo kwa DPP kwa ajili ya kupitiwa, hivyo kutokana na hali hiyo tunaomba tarehe nyigine kwa ajili ya kutajwa ” alidai Magoho.

Hakimu Chaungu, ameahirisha kesi hiyo hadi Machi 23, itakapotajwa na mshtakiwa amerudishwa rumande kutokana na shtaka la mauaji linalomkabili kutokuwa na dhamana kwa mujibu wa sheria.

Katika kesi ya msingi, Luwongo anakabiliwa na kesi ya mauaji namba 4/2019 iliyopo mahakamani hapo.

Anadaiwa kuwa Mei 15, 2019 katika eneo la Gezaulole, wilaya ya Kigambo, mshtakiwa alimuua mkewe aitwaye Naomi Marijani.

Chanzo: mwananchi.co.tz