Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Anayedaiwa kumuua mkewe, kumchoma moto ashikiliwa polisi

67132 Pic+mdada

Wed, 17 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam nchini Tanzania linamshikilia Khamis Luwonga maarufu Meshack mkazi wa Kigamboni kwa tuhuma za  kumuua mkewe, Naomi Marijani.

Luwonga anadaiwa aliuchoma moto mwili wa mkewe.

Mkuu wa Upepelezi wa kanda hiyo,  Camillius Wambura akizungumza na Mwananchi leo Jumatano Julai 17, 2019 amesema wanamshikilia kwa mahojiano kuhusu tukio hilo.

Amesema pamoja na kumhoji polisi wamekwenda katika maeneo ambayo ameyataja kufanya mauaji hayo kwa ajili ya kupata uthibitisho.

“Huyu bwana tunaye tunaendelea kumhoji na askari wameshakwenda katika maeneo aliyoyataja, wamechukua majivu kwa ajili ya vipimo vya DNA kuona  kama kweli yanaendana na huyo mama,” amesema

Joseph Hatia, shemeji yake Naomi amedai kumekuwa na taarifa kuwa Naomi  na mumewe hawakuwa na maelewano mazuri hadi siku anatoweka.

Pia Soma

Amesema kwa taarifa walizozipata Meshack ameeleza kwamba siku ya tukio alirudi nyumbani na kumkuta mkewe lakini waligombana.

 “Wakiwa wanagombana na kusukumana amedai kwamba Naomi alidondoka na kujigonga kichwani, alivyoona hivyo akamburuza hadi nje na kuchimba shimo akamtumbukiza na kuchoma moto.”

Hatia amesema kwa sasa familia inasubiri taarifa rasmi kutoka kwa polisi ambao wanaendelea kumshikilia Luwonga.

Naomi alitoweka nyumbani kwake Mei 15, 2019 na familia yake ilitoa taarifa polisi katika kituo cha Chang’ombe baada ya mumewe kuwajulisha siku nne tangu atoweke.

Chanzo: mwananchi.co.tz