Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Anayedaiwa kumuingiza nyeti mtoto mdomoni kuhukumiwa

91432 Pic+hukumu Anayedaiwa kumuingiza nyeti mtoto mdomoni kuhukumiwa

Fri, 10 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mahakama ya Wilaya ya  Kinondoni Dar es Salaam nchini Tanzania imepanga Januari 20, 2020 kutoa hukumu kwa mshtakiwa Liziki Kessy  anayekabiliwa na shtaka  la kumwingiza uume wake mdomoni  mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka saba ili aunyonye.

Kesi hiyo ilikuwa imepangwa kwa ajili ya kuendelea na ushahidi kwa upande wa utetezi lakini ilishindwa kuendelea baada mshtakiwa huyo kudai hana shahidi.

Kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Hudi Hudi  ilimtaka Kessy amwite shahidi anayemtetea ndipo mshtakiwa huyo akadai aliyekuwa akimtegemea yupo nje ya mkoa hivyo gharama ya  kumsafirisha kuja jijini Dar es Salaam ni kubwa.

Wakili wa Serikali, Daisy Makakala leo Ijumaa Januari 10, 2020 amedai shauri lilikuja kwa ajili ya kuendelea kusikiliza utetezi kutokana na shahidi kutokuwapo aliiomba mahakama hiyo ipange tarehe kwa ajili kusoma hukumu.

Hukumu hiyo inatarajiwa kutolewa baada ya upande wa mashtaka kuita mashahidi watano huku upande wa utetezi ukileta mashahidi watatu akiwemo mshtakiwa mwenyewe.

Kesi ya msingi mshtakiwa anadaiwa kutenda kosa la shambulio la aibu, Julai 24 mwaka 2018 maeneo ya Kimara Stop Over Dar es Salaam mshtakiwa ulimwingizia uume wake mdomoni na katika njia ya haja kubwa mtoto wa kiume wa miaka saba.

Chanzo: mwananchi.co.tz