Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Riziki Pembe Juma ameiomba Jamii Kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kuhakikisha wanatoa taarifa za Mtuhumiwa aitwaye Kheri Mkombe Abdallah ambaye anatuhumiwa kumuingilia mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka kumi na moja Kinyume na Maumbile.
Waziri Riziki ametoa ombi hilo wakati akizungumza na Waandishi wa habari katika kikao chake kilichofanyika katika Ukumbi wa Nyumba za Wazee Sebleni MJini Unguja.
Amesema ni vyema wananchi wakatoa ushirikiano wa kutoa wa kumbaini mtuhumiwa huyo sehemu aliyojificha ili akamatwe na kufikishwa katika vyombo vya sheria kwa kujibu shtaka hilo. Tukio hilo la kumuingiliwa mtoto wake wa kumzaa linadaiwa kutokea Mei 11, Mwaka huu Majira ya saa nne usiku.