Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Anayedaiwa kumbaka binti yake akutwa na kesi ya kujibu

Mtuhumiwa Kumbaka Mwanaye.png Anayedaiwa kumbaka binti yake akutwa na kesi ya kujibu

Tue, 12 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita imemkuta na kesi ya kujibu mkazi wa kijiji cha Masumbwe wilayani Mbogwe,Thomas Sitta baada ya upande wa mashtaka kufunga ushahidi wa shtaka la ubakaji linalomkabili.

Mshtakiwa huyo katika kesi namba 62/2023, anashtakiwa kwa kosa la kumbaka mtoto wake wa kambo mwenye umri wa miaka 13 ambapo alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Mei 10, 2023.

Uamuzi huo umetolewa leo Septemba 11, 2023 na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo, Johari Kijuwile baada ya kusikiliza ushahidi uliowasilishwa na askari wa idara ya upelelezi mwenye namba G378 Sajenti Masuka.

Akitoa ushahidi wake Sajenti Masuka ameieleza Mahakama kuwa Aprili 4 ,2023 akiwa kazini alipeewa jalada la kufuatilia lenye namba KCW/IR110/2023 likiwa na tuhuma za ubakaji akitakiwa kuendelea na upelelezi.

“Niliposoma jalada nilibaini mtuhumiwa yupo mahabusu na ‘victim’ (mwathirika) akiwa maeneo ya kituo cha polisi Geita niliongea na Victim faragha na kunieleza namna alivyobakwa na baba yake wa kambo huko Rubanga, nilizungumza pia na mshtakiwa na alikiri kumbaka mtoto wake,”amesema

Akiongozwa na Wakili wa Serikali, Venance Mkonongo, Shahidi huyo ameieleza Mahakama kuwa alikwenda pia kwenye nyumba ya wageni alikokamatwa mtuhumiwa akiwa kwenye chumba kimoja na mwanae na kufanya mahojiano na wahudumu waliokuwepo siku ya tukio ambao walieleza kushangazwa na mshtakiwa kuingia chumba kimoja na mtoto na kuamua kuita watu waliofanikiwa kumkamata.

Alipopewa nafasi ya kuuliza swali kabla ya hakimu kutoa uamuzi Mshatakiwa amedai hajawahi kumuona mpelelezi huyo na wala hakuwahi kuhojiwa wala kukiri kosa na kwamba toka akamatwe hakutoka nje ya mahabusu hadi siku aliyotolewa na kupandishwa Mahakamani.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 25, 2023 itakapokuja kwa ajili ya mshtakiwa kujitetea mwenywe baada ya kudai hana mashahidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live