Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Anayedaiwa kulawiti naye alawitiwa mahabusu!

Mahabusu Pc Data Anayedaiwa kulawiti naye alawitiwa mahabusu!

Thu, 30 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Firauni, msemo unajidhihirisha baada ya kijana mmoja wa kiume miaka 22 aliyeshikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kufanya ulawiti hivi karibuni, naye yeye kunaswa na tuhuma za kufanyiwa ulawiti akiwa mahabusu ya Polisi na Mahabusu mwenzake mwenye umri wa miaka 40

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini magharib Unguja Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Richard Thadei Mchomvu ameeleza hayo mbele ya waandishi wa habari huko ofisini kwake Mwembe madema Mjini Unguja wakati waandishi walipotaka kufahamu juu muendelezo wa watuhumiwa wa ulawiti waliotajwa wiki iliyopita na kushikiliwa na Jeshi hilo

Amesema kikawaida askari polisi hufanya doria kila baada ya saa moja katika mahabusu hizo lakini tukio la kitendo hicho kimeripotiwa na mmoja ya mahabusu aliyekuwemo ndani ya kituo hicho na kuita askari na kudai kuwa mahabusu mmoja anamlawiti mahabusu mwenzake

Aidha amesema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa kesi hiyo ili kuongeza shtaka dhidi yao juu ya makosa waliyoyafanya kwa nyakati tofauti

Chanzo: www.tanzaniaweb.live