Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Anaswa na meno ya tembo

Tembo Pic Data Kamanda Musilim akionyesha meno yaliyodakwa

Tue, 12 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro kwa kushirikiana na jeshi la hifadhi ya taifa ya wanyamapori ya Nyerere (Tanapa) inamshikilia mkazi wa Duthumi katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Semeni Mrisho (49) kwa tuhuma za kupatikana na vipande 18 vya meno ya tembo mkoani hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Fortunatus Musilimu amesema mkazi huyo alikamatwa April 8, 2022 katika Kijiji cha Mngeta baada ya askari kupata taarifa kutoka kwa msiri wao iliyosaidia kukamatwa na meno vipande 18 vikiwa ndani ya mfuko wa kiroba akielekea kwenda kuviuza.

Kamanda Musilimu amesema thamani ya meno hayo bado haijafahamika na uzito wake na wanaendelea na uchunguzi kubaini mtandao huo.

“Mtuhumiwa tulipomhoji mbele ya Mwenyekiti wa kijiji cha Nyandila, Raymond Simba amekiri kupatikana na vipande 18 vya meno ya tembo na kwa siku tofauti tofauti amekuwa akiingia katika hifadhi ya wanyamapori ya Nyerere kuua tembo na kuchukua meno yao.”amesema Kamanda Musilimu.

Kamanda huyo amesema mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa na mara baada ya kukamilika kwa upelelezi atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi.

Kaimu mkuu wa hifadhi ya taifa ya wanyamapori Nyerere, Khalid Mngofi amesema wamefanikiwa kukamata vipande 18 vya meno ya tembo ikiwa ni mmoja ya mtandao wa uhalifu wa ujangili wa kuua tembo huku mtandao huo ukisakwa kwa muda mrefu bila mafanikio. Mngofi amesema mtandao wa ujangili wa kuua tembo umeanza kurudi na wao kama askari wenye thamani wa kulinda wanyamapori wamejipanga kufanya doria na kuwakamata.

“Tuna mikakati tukishirikiana na askari wa jeshi la polisi na tumeimarishi kitengo cha taarifu fiche kwa ajili ya kupata taarifa za viashiria vya uwepo wa wahalifu kabla ya kutekeleza azma yao na kuwachukulia hatua kwa manufaa ya kizazi chetu na kijacho.”amsema

Ameongeza kuwa ujangili mdogo mdogo umepungua kwa kiasi kikubwa na ujangili unaofanyika ni pale wanyama wanapotoka hifadhini na kuingia katika hifadhi ya misitu ya vijiji na baadhi ya wananchi kuwaua kwa ajili ya kitoweo na wanapopata taarifa wanachukua hatua kwa wahusika.

Wakati huohuo, Jeshi hilo linamshikilia mkazi wa kijiji cha Kibedya tarafa ya Gairo wilayani Gairo, Hussein Chidaga (53) kwa tuhuma za kuvunja madirisha vioo vya madirisha 12 katika madarasa ya shule ya sekondari Kibedya.

Kamanda Musilimu amesema mkazi huyo alitekeleza tukio hilo kama njia ya kulipa kisasi kwa mlinzi aliyekuwa akilinda shule hiyo baada ya kumtuhumu kutembea na mke wake. “Jeshi la Polisi lilifanya uchunguzi na kubaini kuwa mtuhumiwa alikuwa na lengo la kulipa kisasi kwa mlinzi huyo kutembea na mke wake na baada ya kumkosa alichukua maamuzi ya kufanya uhalifu huo lakini jeshi la polisi limeweza kumtia nguvuni na atafikishwa katika vyombo vya sheria kwa hatua zaidi.”amesema Kamanda Musilimu.

Katika tukio lingine, Kamanda Musilimu amesema katika operesheni ya kuzuia uhalifu wa aina mbalimbali, imewakata watuhumiwa watatu kwa makosa ya kuzalisha, kusambaza na kuuza vinywaji bandia aina ya smart Gin na stika mpya zenye nembo ya mamlaka ya mapato Tanzania (TRA).

Kwa mujibu wa Kamanda Musilimu watuhumiwa hao wanamiliki kiwanda cha kutengeneza vinywaji hivyo bandia aina ya Smart Gin na Rivella kilichopo eneo la Kichangani Manispaa ya Morogoro na baada ya kufanyia upekuzi walikutwa na vifaa mbalimbali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live