Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Anaswa akiuza mtoto wake wa siku tano akatengeneze pua

MTOTO AKIUZWA M.jpeg Pichani mwenye plasta ndie aliyezaa na huyo mwingine ndie mnunuzi.

Mon, 18 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamke mmoja ambaye jina lake halijaanikwa wazi amekamatwa na kushtakiwa baada ya kukutwa akimuuza mwanaye wa kiume kumzaa mwenye umri wa siku tano, huko Dagestan, jiji la Kaspiysk, Kusini mwa Urusi.

Mdada huyo mwenye plasta (33) amesema alitaka kumuuza mwanaye huyo ili apate pesa za kwenda kufanya sajari kurekebisha pua yake hiyo ili azidi kuwa mzuri zaidi.

Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari na polisi wa Urusi, mrembo huyo baada ya kuzaa alimwambia rafiki yake hana nia ya kulea mtoto mchanga. Tayari wanashtakiwa kwa makosa kwa biashara hiyo haramu ya kuuziana watu.

Tayari mama huyo alishazungumza na mwanamke na mwanaume (couple) waliokuwa wameshatoa fedha kiasi ili kumnunua mtoto husika ambapo jumla walikubaliana manunuzi hayo yawe £2900 ambazo sio chini ya milioni 7.9 za Tanzania lakini walimpa asilimia 10 tu ya malipo yote (£274).

Wapenzi waliotaka kununua mtoto huyo aliyezaliwa Aprili 25, 2022, wakati wakihojiwa na polisi wamesema, awali mdada huyo pichani aliwaambia hana kazi wala sehemu ya kuishi ndio anahitaji pesa.

Baada ya kuwapa mtoto, aliugua wakampeleka Caspian City Central Hospital, walipofika walihojiwa cheti cha mtoto lakini hawakuwa nacho, waliporudi kwa huyo mama halisi wa mtoto kumuuliza kuhusu cheti cha mtoto akawataka wamalizie malipo yaliyobaki ndipo awape cheti.

Baada ya kupokea pesa hizo Mei 26, 2022, mama aliwawaambia pesa hizo za kumuuza mwanae amepanga akafanye sajari ya pua ili kuongeza ubora wa urembo wake. Lakini pia hana kazi wala mahali pa kuishi, hivyo zitamsaidia katika maisha yake.

Na kabla hawajamalizana kulipana malipo ndio wote watatu wakadakwa na vyombo vya sheria kwa biashara hiyo haramu ya kuuziana watu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live