Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Amuua wifi yake kisha kumkatakata vipande na kuvitia kwenye begi

Mauaji Wifi.jpeg Amuua wifi yake kisha kumkatakata vipande na kuvitia kwenye begi

Sun, 28 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamke huyo wa nchini Cameroon kwa jina la Merie France Mbea (57) ametiwa nguvuni na vyombo vya dora kwa tuhuma za kumuua wifi yake ili apate utajiri baada ya kuambiwa afanye hivyo na mwanaume aliyekuwa akiwasiliana nae.

Tukio limetokea tarehe 22 Agosti, 2022, ambapo amemuua wifi yake hotelini kwa kumpiga kichwani na chupa ya bia kumpasua koo kisha kumkatakata vipande vipande na kuvifunga kisha kuvitia kwenye begi kubwa.

Wakati wa kutoka hotelini wahudumu walimuona amebeba mzigo mzito sana wakataka kumsaidia ndipo akakataa na kusababisa wahudumu kuingiwa na wasiwasi na kuwaita polisi.

Akihojiwa na polisi amesema mwanaume husika ambaye hajafahamika mara moja ndiye aliyemuagiza apeleke viungo vya wifi yake ili apate utajiri.

Pichani anavyoonekana ni baada ya kuwekwa chini ya ulinzi akiwa na vipande vya wifi yake kwenye begi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live