Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Amuua mpenzi wake akidai amemsaliti, naye ajiua

32214 Pic+mauaji TanzaniaWeb

Tue, 18 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Bukoba. Mwalimu wa Sekondari ya Nyanshenye Manispaa ya Bukoba, Karoli Domisian (36) amemuua mpenzi wake, Regina Temu (29) kisha naye kujinyonga hadi kufa kwa kutumia kamba ya manila akidai kuwa amesalitiwa.

Akizungumza leo Jumanne Desemba 18, 2018 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Revocatus Malimi amesema miili ya wapenzi hao imegundulika katika chumba kimoja huku mwalimu huyo ikidaiwa ameacha ujumbe wa maandishi.

Amesema Regina ambaye alikuwa mfanyakazi wa kiwanda cha kukoboa kahawa cha Tanica alinyongwa kwa tai na ndani ya chumba hicho ukakutwa mwili wa mwalimu huyo.

Katika tukio hilo la Desemba 17, 2018 Kamanda Malimi amesema ujumbe wa maandishi ulioachwa na mwalimu huyo unaeleza kuwa amechukua uamuzi huo baada ya mpenzi wake huyo kumsaliti.

Amesema Regina aliyekuwa akiishi na dada yake aliondoka nyumbani tangu Desemba 16, 2018 na hakurejea hadi mwili wake ulipoonekana akiwa tayari amefariki dunia.

Amesema katika uchunguzi wa awali wamebaini marehemu hao hawakuwa kwenye uhusiano kwa muda mrefu.



Chanzo: mwananchi.co.tz