Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Amuua mkewe na kuuchoma moto mwili wake

Kifo Mauaji Wachimbaji Madini?fit=640%2C426&ssl=1 Amuua mkewe na kuuchoma moto mwili wake

Sun, 28 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi huko Nyandarua wanamzuilia mwanamume mmoja kwa tuhuma za kumuua mke wake kikatili, na kuuchoma na moto mwili wake.

Kulingana na ripoti ya polisi, Titus Nderitu Gichohi, anadaiwa kumuua mkewe nyumbani kwao kabla ya kutumia gari lake kusafirisha maiti hadi Kijiji cha Pesi, eneo bunge la Ndaragua, ambapo inadaiwa aliiuchoma moto ili kuharibu ushahidi wowote ambao ungemhusisha na mauaji.

''Uchunguzi wa matukio hayo unaonyesha kuwa mwathiriwa aliuawa ndani ya nyumba yake na mwili wake kuhamishwa hadi eneo jingine ambapo mshukiwa aliuchoma katika juhudi za kuharibu ushahidi,” Ripoti ya polisi imesema.

Awali polisi walikuwa wakichukulia kisa hicho kama kisa cha utekaji nyara kabla ya wakaazi wa eneo hilo kutoa taarifa kwamba walikuwa wameona gari la marehemu nyumbani kwa Gichohi.

Hili liliwafanya wapelelezi kuzuru eneo la tukio, ambapo walikuta mwili wa marehemu ukiwa bado unawaka moto na kuchomeka kabisa.

Kulingana na Naibu Kamishna wa Kaunti Ndogo ya Aberdare Charles Rukwaro, mshukiwa hakuwa katika eneo la tukio wakati huo lakini inasemekana alikamatwa na polisi eneo la Kasarani alipokuwa akijaribu kutoroka. Mwili wa marehemu umehamishiwa katika hospitali ya Nyahururu kaunti ya Laikipia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live