Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Amuua mkewe akimtuhumu kumharibu nguvu za kiume

58767 Pic+amuua

Tue, 21 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tabora. Dumala Kalimba (45), mkazi wa kata ya Ntobo wilayani Igunga Mkoa wa Tabora anatuhumiwa kumuua mkewe kwa kumkata na panga kichwani kwa madai kuwa amemroga uume wake usifanye kazi.

Akizungumza leo Jumanne Mei 21, 2019 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Emmanuel Nley amesema tukio hilo limetokea jana saa sita mchana katika kijiji hicho.

Amesema mtuhumiwa alimvizia mkewe alipokuwa nyumbani na kumpiga panga kichwani, kwamba polisi wanamshikilia kwa mahojiano zaidi.

Kamanda Nley amesema uchunguzi wa awali unaonesha mtuhumiwa alikuwa akimtuhumu mkewe kuwa amemroga kwa kuwa uume wake haukuwa ukifanya kazi.

Nley amewataka wakazi wa Tabora kutoendekeza ushirikina na kujichukulia sheria mkononi.

Wakizungumzia tukio hilo mkazi wa Kanyenye manispaa ya Tabora, Aidan Musa amewataka wakazi wa mkoani humo kuishi katika misingi ya dini na kuacha kuamini ushirikina.

Pia Soma

Maulid Juma, mkazi wa Isevya amesema mwezi wa Ramadhan ni kipindi cha mafunzo mbalimbali na kwamba wananchi wanatakiwa kuichi kwa imani.

Chanzo: mwananchi.co.tz