Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Amuua mkewe, akata sehemu za mwili kutunza kwenye friji

Mauaji Mdsf.jpeg Amuua mkewe, akata sehemu za mwili kutunza kwenye friji

Tue, 28 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mume wa zamani na wakwe wamekamatwa na kushtakiwa kwa uhalifu kuhusiana na kifo cha mwanamitindo Abby Choi huko Hong Kong.

Mwanamitindo huyo mwenye makazi yake Hong Kong, 28, alionekana mara ya mwisho katika eneo la Tai Po jijini humo siku ya Jumanne.

Siku ya Ijumaa, polisi waliingia katika nyumba moia ya wageni na kupata mabaki ya binadamu, ambayo baadaye yalitambuliwa kama miguu ya Choi, kwenye friji.

Baadhi ya mali za Choi pia zilipatikana katika chumba hicho, ikiwa ni pamoja na kadi yake ya bank na kitambulisho, kulingana na mtangazaji aliyekuwemo karibu na eneo hilo RTHK.

Alan Chung, msimamizi wa idara ya polisi ya mkoa, aliwaambia waandishi wa habari kuwa sio sehemu zote za mwili wa Choi zilizogunduliwa kwani sehemu za mwili ambazo tulipata zilikuwa ndani ya friji na kulikuwa na miguu miwili ya mwanamke,” Chung alisema, kulingana na RTHK.

“Bado tunatafuta kichwa pia kuna viungo vingine vya mwili havipo kwa mfano eneo la kiwiliwili, mikono hivyo tunaamini mtuhumiwa ameshatoa viungo vya mwili tayari.

Polisi baadaye walithibitisha Jumapili kwamba fuvu la kichwa na mbavu kadhaa zilipatikana kwenye chungu cha kupikia kwenye friji katika makazi hayo hayo ya Tai Po ambapo viungo vingine vya mwili viligunduliwa hapo awali.

Kwa mujibu wa RTHK, polisi walisema kuwa wataalamu wa uchunguzi wa kitaalamu waligundua shimo kwenye fuvu la kichwa ambalo lilisababishwa na kitu kigumu, ambacho kinaaminika kuwa chanzo cha kifo chake.

Siku ya Jumatatu, wanafamilia hao wanne walifika mahakamani, ambapo Alex, kaka yake na baba yake wote walishtakiwa kwa mauaji ya Choi, huku mama yake akishtakiwa kwa kupotosha taarifa kuhusu mkwe wake.

Wanne hao waliwekwa kizuizini bila dhamana, kulingana na shirika la Associated Press na hawajawasilisha ombi lolote na kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 8 ili kutoa nafasi kwa uchunguzi zaidi wa mauaji ya Choi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live