Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Amuua mke na mwanawe

Peter Nielsen Amuua mke na mwanawe

Mon, 23 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Peter Nielsen; ni raia wa Denmark ambaye amehukumiwa kifo nchini Nigeria baada ya kukutwa na hatia ya kumuua mkewe na mtoto wao wa kike wa miaka mitatu.

Mahakama jijini Lagos imesema mwendesha mashtaka amewasilisha ushahidi wa kutosha kumtia hatiani Peter ambaye amehukumiwa kunyongwa hadi kufa.

Mshtakiwa alikana kuhusika na mauaji hayo wakati kesi ikiendelea mahakamani. Mauaji hayo yalifanyika Aprili 5, mwaka 2018 katika nyumba ya wanandoa hao katika kitongoji tajiri cha Banana Island jijini Lagos.

Kesi hiyo iliibua hisia ya umma hasa kutoka kwa makundi ya kutetea haki za wanawake.

Hukumu ya kifo kwa kunyongwa ndiyo adhabu kuu kwa kosa la mauaji nchini Nigeria; nchi ya Afrika Magharibi yenye watu zaidi ya milioni 212.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live