Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Amuua mke, mtoto nae ajiua

WhatsApp Image 2021 03 30 At 16.13.12.jpeg Amuua mke, mtoto nae ajiua

Tue, 30 Mar 2021 Chanzo: ippmedia.com

Kamanda wa polisi mkoani Kagera Revocatus Malimi amesema kuwa tukio hilo lilitokea Machi 26 mwaka huu saa 09 usiku,  na kuwataja waliopoteza maisha kwa kukatwa mapanga kuwa ni Editha Martine (48) na binti yake Sawia  Sudi (25) baada ya kubadilisha dini kutoka Uislamu na kuwa Wakristu.

"Kitendo cha mke wake na binti yake kubadilisha dini inaonekana kilimkasirisha baba mwenye nyumba, baada ya mama kuona ugomvi hauishi aliamua kuhamia sehemu nyingine akiwa na binti yake, na wakati wakiishi huko usiku walivamiwa na mtuhumiwa ambaye aliwashambulia kwa panga na kusababisha vifo vyao papo hapo" amesema.

Amesema kuwa baada ya baba huyo kutekeleza mauaji hayo alijinyonga kwa kutumia shuka, alilolifunga katika tawi la mti, na kuwa jeshi hilo limeanza kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo.

Chanzo: ippmedia.com