Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ampiga mawe 'ex' wake hadi kufa

Fisi Mauaji?fit=613%2C356&ssl=1 Ampiga mawe aliyekuwa mpenzi wake hadi kumuua

Fri, 14 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi nchini Afrika Kusini linamsaka mwanaume ambaye bado hajafahamika kwa majina kwa tuhuma za mauaji ya aliyekuwa mpenzi wake kwa kumpiga na mawe katika jimbo la Limpopo lililopo Kaskazini mwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa tovuti ya The South African, tukio hilo lilitokea Jumamosi majira ya asubuhi katika kijiji cha Dzingidzingi, ambapo muuaji alitekeleza kitendo hicho alipokutana njiani na mpenzi wake aitwaye Nokuthula Sithole (23) ambaye pia ni mama wa mtoto wake.

Msemaji wa Polisi wa Limpopo Kanali Malesela Ledwaba, amesema marehemu Sithole alikuwa pamoja na rafiki yake ambao walikuwa wakielekea nyumbani, ndipo wakakutana na muuaji huyo.

Ledwaba amesema, “Inadaiwa wawili hao walizozana kabla ya mshukiwa kumpiga muathiriwa kwa mawe. Rafiki yake alipiga kelele kuomba msaada na akakimbia katika nyumba zilizokuwa jirani.”

Rafiki yake aliporudi alikuta kajeruhiwa vibaya na kupoteza fahamu. Sithole alifariki baada ya kukimbizwa hospitali.

Polisi wa eneo hilo walipewa taarifa, kesi ya mauaji ikafunguliwa na msako mkali ulianzishwa, pia walitoa taarifa mwanaume huyo ajisalimishe katika kituo cha polisi kilicho karibu yake.

Katika kisa kingine cha hapo Limpopo, mwanaume mmoja amejisalimisha kwa Polisi kwa kosa la kumchoma kisu mpenzi wake hadi kumuua.

Mshukiwa huyo anadaiwa kumchoma kisu mpenzi wake mwenye umri wa miaka 27, Aprili 8 kisha kutokomea kusikojulikana.

Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi inadaiwa alikamatwa baada ya maafisa kuibana familia yake ambayo ilitoa taarifa kuonyesha sehemu aliyokuwa kajificha ambayo ni msituni, hivyo akajisalimisha kwa hiari.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live