Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Amnajisi mwanafunzi na kumuua

Eb100a590d4dedbbef2734cfbcf19c8e Kamanda wa Polisi Mkoa Pwani, Pius Lutumo

Thu, 2 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi Mkoani Pwani wanamsaka mtu mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa, mwenye umri kati ya miaka (30) na (40) kwa tuhuma za kumnajisi na kumuua kwa kumziba na chandarua mdomoni mwanafunzi wa darasa la pili mwenye umri wa miaka (7), aliyekuwa anayesoma shule ya Msingi Misugusugu.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa Pwani, Pius Lutumo, mtuhumiwa alitendea tukio hilo nyumbani kwake, Mei 30 mwaka huu Mtaa wa Vitendo Misugusugu, Kata ya Misugusugu wilayani Kibaha, ambapo baada ya tukio hilo mtuhumiwa alitoroka.

"Uchunguzi wa awali umebaini mtuhumiwa alifanya tukio hilo la mauaji, wakati akimbaka mwanafunzi huyo, ambapo alimziba mdomo kwa kutumia chandarua, ili asipige kelele huku akimbaka na kusababisha kifo hicho," amesema Lutumo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live