Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Amfumania mkewe, ampa kichapo mgoni wake, wakamatwa wote na polisi

Amfumania Mkewe, Ampa Kichapo Mgoni, Wakamatwa Wote Na Polisi Amfumania mkewe, ampa kichapo mgoni wake, wakamatwa wote na polisi

Thu, 29 Feb 2024 Chanzo: millard

Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Zanzibar wanawashikilia watu wawili akiwemo aliyechukua mke wa mtu na aliyechukuliwa mke wake kutokana na kujichukulia hatua mikononi baada ya kumfumania mkewe na mwanaume mwingine aitwae Mundhir Khamis Karama (32).

Mundhir anadaiwa kumchukua Mwanamke na kumpeleka nyumbani kwake huko Kijichi ambapo baada ya muda mfupi wakiwa chumbani alivamiwa na Watu watano ambao mmoja wao alidai kuwa Mume wa mwanamke huyo ambapo inadaiwa Watu hao walimshambulia kwa fimbo na vitu vyenye ncha kali kisha kumfunga kitambaa usoni na kuondoka nae.

Imedaiwa kuwa Watu hao walimpora Mundhir simu yenye thamani ya Tsh.400,000 pamoja na kisha kumtaka apige simu kwa Ndugu zake ili watume pesa ndipo aachiwe kitu ambacho Polisi wamesema ni moja ya sababu za Mume Mtu kukamatwa kwa sababu huo ni uhalifu.

Jeshi la Polisi limesema lilifanya msako mkali na kufanikiwa kuwakamata Watuhumiwa walioshiriki tukio hilo ambao ni Mume (Khamis Seif Khamis Mume - 30) na Mke wake (aliyekutwa ndani ya chumba na Mundhir) ambapo juhudi za kuwakamata Watuhumiwa wengine zinaendelea.

Chanzo: millard