Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Amdunga kisu na kumuua mdogo wake wakigombania kuku

Kisuuu Amdunga kisu na kumuua mdogo wake wakigombania kuku

Tue, 19 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanaume mmoja anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kumchoma kisu na kumuua kaka yaake katika kaunti ya Kakamega nchini Kenya.

Kisa hicho kilichofanyika katika kijiji cha Senyende ambapo mwanaume Bonaventure Lumwachi, 37, anadaiwa kumdunga kisu na kumsababishia umauti mdogo wake Augustine, 35, baada ya ugomvi kuhusu kuku aliyepotea.

Ndugu zao walisema mshtakiwa alimvamia kaka yake na kumchoma kisu chenye ncha kali kifuani baada ya ugomvi wa mahali alipo kuku huyo. Mwili wa marehemu ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya eneo hilo.

Kamanda wa Polisi wa Kaunti ndogo ya Shinyalu Robert Makau alisema wanakijiji waliokuwa na hasira walimvamia mshukiwa wa mauaji hayo kabla ya kuokolewa na kupelekwa hospitalini.

Hivyo amelazwa katika hospitali kuu ya kaunti ya Kakamega akiwa katika hali mahututi.

“Mshukiwa anaendelea kupokea matibabu katika Hospitali Kuu ya Kaunti ya Kakamega. Atashtakiwa kwa mauaji mara tu atakaporuhusiwa kutoka hospitalini," alisema Makau.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live