Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Amchinja mwanaye kwa msumeno

Mauaji Mtoto Ms.jpeg Amchinja mwanaye kwa msumeno

Fri, 1 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Gabriel Volts anashikiliwa na vyombo vya sheria baada kumchinja kwa msumeno mwanaye wa mwaka mmoja na miezi nane ili awe tajiri.

Gabriel mwenye umri wa miaka 33 ni rai wa Nigeria ambaye anadaiwa kumtenganisha kabisa mwanaye kichwa na kiwiliwili.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka nchini humo, Juni 24, mwaka huu, mama wa mtoto husika hakumuona mwanaye kwa muda mrefu.

Alipomuuliza baba mtoto huyo aliko mtoto wao, Gabriel akasema kuwa alimpeleka kwa dada yake eneo linaloitwa Wari.

Mama wa mtoto alikwenda huko kwa wifi yake, lakini alipofika hakuona mtoto wala nini na kujua kuwa amedanganywa.

Mama wa mtoto akaingiwa na wasiwasi na kwenda kutoa taarifa Polisi ambapo walifika na kumtia mbaroni baba mtoto.

Mwanaume huyo alipohojiwa na Polisi alikiri kumuua mwanaye huyo. Gabriel alisema aliota ndoto mtu anamjia akamwambia ukimuua mwanao na kuipaka damu yake kichwani utakuwa tajiri.

Hapo ndipo alimchukua mwanaye hadi kichakani akamchinja kwa msumeno kichwa akakifukia pembeni ya mti wa mtende kisha akakitupa porini kiwiliwili cha mwanaye ambacho alikikata mikono pia.

Kwa sasa anasubiri sheria ichukue mkondo wake baada ya Polisi kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live