Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ambaka mtoto wa shemeji yake, afungwa jela miaka 30

Ambaka Mtoto Wa Shemeji Yake, Afungwa Jela Miaka 30 Ambaka mtoto wa shemeji yake, afungwa jela miaka 30

Thu, 13 Jun 2024 Chanzo: Millard

Mahakama ya Wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro imemuhukumu kifungo cha miaka 30 jela Mkazi wa Chakwale, Michael Mchanjale (31) baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumbaka Mtoto wa Shemeji yake mwenye umri wa miaka 15 ambaye ni Mwanafunzi wa kidato cha kwanza na kumuharibia bikra yake.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mwanadamizi Mfawidhi, Irene Lyatuu amesema Mshtakiwa huyo ametiwa hatiani kwa kosa hilo la ubakaji ambapo amehukumiwa kwenda jela miaka 30, huku rufaa ikiwa wazi endapo hajaridhika na hukumu.

Hakimu Irene amesema Mshtakiwa alitenda kosa hilo September 22,2023 baada ya Binti huyo kufika nyumbani kwa Mtuhumiwa ambaye ni Baba yake mdogo kutokana na Mama yake wa kambo kumfukuza nyumbani kwa kosa la Binti huyo kuchelewa kurudia ambapo baada ya kufika hakufanikiwa kumkukuta Mama yake mdogo badala yake alimkuta Mtuhumiwa (Baba yake mdogo) majira ya saa tatu usiku.

“Baba huyo alimgongea mlango majira ya usiku na alipoingia ndani alizima taa kisha kumvua nguo na kumziba mdomo baadaye kuchukua uume wake na kuingiza kwenye uke wake na alitumia dakika 20 huku akisikia maumivu makali kwani alikua hajawahi kuingizwa kitu chochote sehemu zake za siri (uke)”

Hakimu Irene amesema mwezi mmoja baada ya kubakwa Msichana huyo aligundulika kuwa na ujauzito na alipoulizwa alidai Baba yake mdogo Michael ndiye aliyembaka usiku na kumtishia asiseme kwa Mtu yoyote la sivyo atamuua, pia ushahidi wa cheti cha Daktari umeonesha Msichana huyo aliingizwa kitu chenye ncha kali sehemu za siri na kuondoa nyama nyama laini.

Hakimu Irene anasema Mtuhumiwa huyo amefikishwa Mahakamani kwa makosa mawili ikiwemo la kubaka na kumpa ujauzito Mwanafunzi ambapo Mahakama hiyo imemtia hatiani kwa kosa moja la kubaka huku ikimuachia huru kwa kosa la kumpa ujauzito hadi ushahidi utakapowasilishwa ikiwemo vipimo vya DNA.

Chanzo: Millard