Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyeua wawili Shinyanga naye auawa

Aliyeua Pichhh Aliyeua wawili Shinyanga naye auawa

Tue, 4 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu wawili wamefariki dunia baada ya kupigwa na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wao na wengine watatu kujeruhiwa na mtu anayedaiwa kuwa na tatizo la akili kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.

Akisimulia tukio hilo leo Oktoba 4, mmoja wa majeruhi hao Daniel Emmanuel, amesema tukio hilo lilitokea Oktoba 2 na kwamba waliouawa ni Nicholaus Leonard na Badmalta Melikiad.

Amesema mtu huyo alivamia katika nyumba ya Leonard na kuanza kushambulia familia hiyo na kwamba yeye amejeruhiwa wakati akiwasaidia wenzake.

“Baada ya kusikia kelele katika nyumba hiyo nilienda kuwasaidia, mtu huyo alikuwa amefunga mlango na mimi nilivyofika nikafungua mlango, lakini bahati mbaya jamaa alikuwa amejibanza katika kona nilivyoingia tu akanipiga kichwani nikaanguka chini.

“Wakati vurugu hizo zikiendelea na mimi kulemewa kushindwa kutoa msaada kutokana na kuvuja damu nyingi, mume wa Lucia Luhende, Nicholaus Leonard aliingia ndani kutoa msaada, lakini na yeye akapigwa kichwani akaanguka chini na kupoteza maisha papo hapo,” amesema Emmanuel amesema.

Mke wa marehemu Lucia Luhende amesema yeye alifanikiwa kutoka nje wakati mtu huyo akiendelea kumshambulia rafiki yake, ndipo mume wake akaingia ndani ili kumuokoa lakini hakufanikiwa kutokana na kupigwa vibaya kichwani kisha akapoteza maisha.

Diwani wa Kolandoto, Mussa Andrew amesema baada ya kupokea taarifa alifika eneo la tukio na kumkutana mtu huyo akiwa bado ndani ya nyumba hiyo, akapiga simu kuomba msaada Polisi.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Kolandoto, Dk Joseph Wallace amethibitisha kupokea miili ya watu watatu akiwamo kijana anayetuhumiwa kuwaua watu hao wawili, ambaye aliuawa na wananchi.

Pia, Dk Wallace amesema mmoja kati ya majeruhi watatu amepewa rufaa kwenda hospitali ya Bugando jijini Mwanza kwa matibabu zaidi.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo la mauaji, na kutoa wito kwa wananchi wakimuona mtu analeta taharuki watoe taarifa kwa wakati ili kuzuia maafa yasitokee.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live