Polisi nchini Canada wametoa ripoti ya mauaji ya watu 11 waliouawa kwa shambulizi la kisi mwezi uliopita.
Mshukiwa wa mauaji ya watu 11 ameleta taharuki nchini humo , haswa kutokana na kuwa kua miongoni mwa watu aliowaua kwa kisu ni kaka yake wa kuzaliwa.
Polisi wa nchi hiyo wamesema kwamba Bw.Myles Sanderson (32) alipoteza maisha wakati akifukuzana na polisi barabarani tarehe 7 mwezi uliopita.
Kaka yake mwenye umri w a miaka 31 alikutwa amepoteza maisha huku watu wengine 10 wakipoteza maisha baada ya shambuilizi hilo baya.
Mauaji ya halaiki nchini Canada ni nadra kutokea, huku wengi wakishangazwa na tukio hilo na wakijiuliza sababu ya kutokea kwake. Tukio hilo lililojiri Septemba 4, 2022, sikukuu ya wafanyakazi nchini Canada, lilisababisha msako mkali wa mtuhumiwa huyo.