Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyeua wapenzi wanne na mtoto atupwa jela miaka 105

Jela 1.jpeg Aliyeua wapenzi wanne na mtoto atupwa jela miaka 105

Wed, 13 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama Kuu  huko Kampala Uganda, imemuhukumu kwenda jela miaka 105 Musa Musasizi (25) kwa kuwaua wapenzi wake wanne na mtoto kwa kuwapiga na kitu kichwani au kuwanyonga kabla ya kuichoma moto miili yao huko Nakulabye.

Musasizi alikamatwa mnamo Machi 25, 2021 na timu ya usalama ya mkuu wa upelelezi wa kijeshi na polisi kufuatia vifo vya wanawake watano na mtoto wa miezi mitatu.  Taarifa inasema Musasizi aliwalazimisha waathirika hao kushiriki kimapenzi na yeye,  kabla ya kuwaua na kuwachoma moto huku miili hiyo akiizika katika eneo moja.

Mwanaume huyo alikiri kutenda mauaji hayo ambapo miongoni mwa sababu alizotaja kuuwa baadhi ya wanawake hao ni mmoja kukataa pesa ya usafiri aliyompa baada ya kushiriki naye kimapenzi kwa madai pesa ni ndogo na mwingine alimuua baada ya kugungua ana mwanaume mwingine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live