Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyeua mtu kwa kucmhoma visu bila kukusudia aachiwa huru

InShot 20230214 181918323 Aliyeua mtu kwa kucmhoma visu bila kukusudia aachiwa huru

Tue, 14 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora imemuachia huru Jonas Charles maarufu Mkondo Abisai, mkazi wa WIlaya ya Sikonge aliyekuwa akikabiliwa na makosa ya kuua bila kukusudia. Jonas alishitakiwa kumuua bila kukusudia kwa kumchoma kisu mara tatu Willson Kaswiza mwaka 2010.

Akisoma uamuzi huo wa mahakama, Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora, Dkt. Mwajuma Kadilu Juma alisema mahakama imepitia hoja za pande zote mbili katika shauri hilo na kubaini kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo bila kukusudia.

Na kwakuwa ameshakaa muda wa zaidi ya miaka sita gerezani ambao unatosha kuwa adhabu, hivyo ameachiwa huru huku akitakiwa kwenda kuishi kistaarabu na jamii pasipo kutenda makosa ya aina hiyo.

Awali upande wa mashtaka chini ya wakili Tunosye Luketa uliiambia mahakama kuwa, mshitakiwa alitenda kosa hilo Juni 22 mwaka 2010 baada ya kumchoma kisu zaidi ya mara tatu marehemu Willson katika vurugu zilizotokea wakati wakiwa kwenye moja ya starehe Kijiji cha Kawale, wilayani Sikonge.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live