Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyetoroka na tiketi ya ndege ahukumiwa miezi mitatu, alipa faini

HUKUMU Aliyetoroka na tiketi ya ndege ahukumiwa miezi mitatu, alipa faini

Tue, 29 Aug 2023 Chanzo: Ethiopia, Saudi Arabia nchi zisizo tumia 'Red Carpet'

Mfanyabiashara Edward Nyerere (35) amehukumiwa kulipa faini ya Sh200,000 au kwenda jela miezi mitatu kwa kosa la kutoweka na tiketi ya ndege yenye thamani ya Sh5 milioni kwenda nchini China, HongKong bila ya kulipia huduma hiyo.

Pia, Mahakama hiyo imemuamuru mshtakiwa huyo kuilipa Kampuni ya kukatisha tiketi za ndege Waheguru Traveling kiasi cha Sh5 milioni.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mfawidhi, Claudis Kipande alisema bila shaka yeyote mahakama imejiridhisha kuwa mshtakiwa amefanya kosa hilo.

"Upande wa mashtaka umethibitisha mashtaka dhidi ya mshtakiwa huyu hivyo inakutia hatiani kwa kufanya kosa hili," alisema Kipande.

Alisema ushahidi uliotolewa na Ofisa Masoko wa kampuni hiyo, Jamila kawawa aliieleza mahakama hiyo kuwa mshtakiwa huyo alienda kwenye ofisi zilizopo jengo la Diamond Plaza, Posta kwa ajili ya kukata tiketi ili asafiri kwenda HongKong.

Kipande alisema kwa maelezo ya ushahidi huo unaeleza kuwa walikubaliana na Ofisa Masoko huyo kuwa mshtakiwa atalipa kiasi kidogo kidogo cha fedha baada ya kupewa tiketi ya ndege alitoweka bila ya kutoa kiasi hicho walichokubaliana.

Hakimu Kipande alimuuliza mshtakiwa huyo kama ana lolote la kuiambia mahakama hiyo ndipo Nyerere alimjibu na kumweleza kuwa ameleta kiasi cha fedha Kwa ajili ya kupunguza deni analodaiwa na Kampuni ya Waheguru Traveling.

Kipande alisema mahakama hiyo inampa adhabu mshtakiwa huyo kulipa faini ya Sh200,000 au kwenda jela miezi mitatu kisha anatakiwa kuilipa Kampuni hiyo kiasi hicho anachodaiwa.

Hata hivyo mshtakiwa alifanikiwa kulipa faini hiyo na kukwepa kifungo cha miezi mitatu jela.

Inadaiwa kuwa Mei 15, 2023 katika Mtaa wa Posta mpya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam Katika jengo la Diamond plaza Katika kampuni hiyo ya kukata tiketi za ndege inayojulikana kwa jina la waheguru Traveling mshtakiwa huyo alijipatia tiketi ya kwenda Hangkong bila kulipa Sh5,000,000 na akatoweka bila kulipa gharama za huduma hiyo

Chanzo: Ethiopia, Saudi Arabia nchi zisizo tumia 'Red Carpet'